Siku moja baada ya Benki ya Dunia kutangaza kusitisha utoaji wa mikopo mipya kwa Serikali ya Uganda baada ya kujiridhisha kuwa sheria ya Nchi hiyo inayopinga ushoga ambayo imelaaniwa na Mataifa mengi ya magharibi ikiwemo Marekani pamoja na Umoja wa Mataifa, inakinzana na maadili ya Beki hiyo, Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema Uganda inaweza kujiendesha na kupiga hatua kimaendeleo bila mikopo.
Museveni amesema “Benki ya Dunia na Waigizaji wengine wanataka kutulazimisha tuache imani, tamaduni, kanuni na Mamlaka yetu ya kujitawala kwasababu ya pesa zao, wanatuweka tabaka la chini Waafrika wote”
“Hatuitaji kupewa presha na Mtu yoyote na kutufundisha jinsi ya kutatua matatizo yetu kwenye Jamii zetu, wao ndio tatizo kubwa kwetu”
Sheria hiyo mpya ya Uganda inatoa hadi hukumu ya kifo kwa ‘ushoga uliokithiri’ ikiwemo kusambaza Virusi Vya UKIMWI kupitia ngono ya mashoga.
Hadi mwishoni mwa mwaka jana 2022, Benki ya Dunia ilitoa dola za Marekani bilioni 5.4 kufadhili miradi ya maendeleo nchini Uganda ikiwemo miradi mingi ya afya na elimu ambayo Benki hiyo inasema inaweza kuathiriwa na sheria mpya iliyopitishwa nchini humo na uamuzi wa kusitishwa kwa mikopo wa Benki hiyo.
Tags
LIFESTYLE