Safari ya ajabu ya miaka 61 ya wanasayansi kutengeneza moyo bandia
Na Sian E Harding
CHANZO CHA PICHA,ELIZABETH FLORES/ALAMY)
Kuanzia chini ya miji mpaka kwenda Mwezini, mafanikio ya uhandisi ya wanadamu ni ya ajabu. Lakini kwa nini kutengeneza moyo wa bandia kumethibitika kuwa vigumu zaidi kuliko ilivyotarajiwa?
Mnamo 1962, John F. Kennedy aliwapa changamoto Jumuiya ya wanasayansi watafute namna ya kumpeleka mtu mwezini na kumrudisha salama duniani mwishoni mwa muongo huo.
Mnamo mwaka wa 1964, daktari wa upasuaji wa moyo na mishipa Michael DeBakey alimshawishi Rais Lyndon B. Johnson kufadhili mpango wa kutengeneza moyo bandia wa kwanza unaoweza kufanya kazi, akianzisha mbio za kwend akufanikiwa kufanya hivyo kabla ya mtu kufika mwezini.
Mnamo mwaka 1969 malengo yote mawili yalionekana kufikiwa, na Taasisi ya Moyo ya Texas iliweza kuweka moyo wa kwanza wa bandia miezi mitatu tu kabla ya kuzinduliwa kwa Apollo 11 ( safari ya mwezini).
Hapo awali, moyo wa bandia ulikuwa na lengo la kuwa mbadala wa moyo halisi unaoshindwa kufanya kazi. Hii ilikuwa hatua kubwa kufikia. Ilikuwa vigumu kuona jinsi moyo bandia unavyoweza kuwekwa kwa mgonjwa na kutarajia aendelee kuishi maisha hata ya kawaida kwa miaka mingi zaidi.
Hata hivyo, historia ya moyo wa bandia pia inaenda sambamba na ile ya upandikizaji wa moyo. Hii ilikuwa ndoto nyingine yenye matumaini makubwa mwanzoni mwa miaka ya 1960, lakini kufikia mwaka 1967 daktari wa upasuaji wa moyo Christian Baarnard huko Cape Town alifanya upandikizaji wa kwanza wenye mafanikio.
Sasa, madhumuni ya moyo wa aina hizi za kwanza za bandia ilibadilishwa. Haikuwa tena kwa ajili ya kumsaidia aishi maisha kama kawaida; kusudi lao likabadilika likawa kumfanya mgonjwa awe hai hadi apatikane wafadhili wa kumpa moyo wa kupandikiza. Kama ilivyo kwa matibabu mengi ya majaribio, kesi ya kwanza ilifanywa kwa mgonjwa ambaye alikuwa amekosa chaguzi. Hakuwa na namna.
Mtu mzima wa miaka 47 alikuwa akifanyiwa upasuaji wa kurekebisha moyo wake uliokuwa umevimba kwenye kuta zake. Alikuwa akisaidiwa na mashine ya kupumua. Ungeondoa mashine angekufa kwa kuwa moyo ulikua dhaifu kabisa. Alihitaji sana kupandikizwa. Denton Cooley, mshirika wa DeBakey, alimwambia kuhusu kumuwekea moyo wa bandia wa majaribio na akakubali. Mgonjwa aliwekwa moyo huo kwa masaa 64 hadi moyo wa wafadhili unaolingana na wake ulipopatikana na kisha kupandikizwa.
Hii ilionekana mwanzoni kama ushindi mkubwa kwa ufanisi wa moyo bandia, lakini kwa kusikitisha mgonjwa alifariki masaa 32 baadaye kutokana na madhara. Kifaa hicho kilikuwa kimeharibu damu na figo zote mbili, na kuta za mifuko hiyo inayoweza kupanuka zilizungukwa na damu iliyoganda. Hii ilitangaza msururu wa matatizo ambayo yangeendelea kuzuia wanasayansi na wahandisi wanaopambana na utaratibu huu.
Moyo wa kwanza uliotengenezwa na Robert Jarvik, moja ya marudio ya wanasayansi yaliyofuata, uliwekwa kwa wagonjwa watano na mmoja aliishi kwa siku 620. Lakini wawili kati ya wagonjwa hao walipata viharusi vikali, na hatimaye wote walikufa kwa madhara au matatizo ya damu.
Maelezo ya picha,
Badala ya kuondoa moyo na kuubalidisha, wataalamu walitengeneza kifaa ambacho kingesaidia kusukuma damu mwilini, kazi inayofanywa na moyo
Upandikizaji wa moyo pia ulianza vibaya, mgonjwa wa kwanza wa kupandikizwa ule wa Baanard alikufa baada ya siku 18 pekee. Mgonjwa wa kwanza nchini Uingereza, ambaye upandikizaji wake ulifanyika katika Hospitali ya Kitaifa ya Moyo ya London, alinusurika kwa siku 45 tu, na kiwango cha kufaulu kwa ujumla kilibaki cha kukatisha tamaa. Tatizo hapa halikuwa namna wanavyofanyiwa upasuaji au utendaji wa awali wa moyo mpya. Ilikuwa ni kutolingana kwa mfumo wa kinga wa mpokeaji wa moyo na ule wa moyo wa wafadhili.
Watu 200 pekee ufanyiwa upandikizaji nchini Uingereza kila mwaka licha ya kuwepo zaidi ya watu 750,000 wenye matatizo ya moyo wanaohitaji upandikizaji, na takwimu zinazofanana hizo zinaonekana duniani kote.
Ili kuziba pengo hili, wanasayansi wamekuwa wakibadilisha vinasaba vya nguruwe ili kuifanya mioyo yao iendane na mfumo wa kinga ya binadamu ili waweze kupandikizwa kwa wagonjwa bila kikwazo. Hii imeonekana kuwa ngumu sana na yenye changamoto, lakini upandikizaji wa kwanza wa kliniki ulianza mnamo 2022.
Mafanikio ya upandikizaji wa moyo, hata hivyo, yaliimarisha utafutaji wa moyo bandia bandia wenye kukamilika, kwa lengo linaloweza kufikiwa zaidi la kumfanya mgonjwa awe hai hadi wafadhili apatikane, au "daraja la kupandikiza" kama inavyoitwa.
Kwa miongo kadhaa, teknolojia ya moyo ya bandia imeboreshwa kupitia mabadiliko ya nyenzo zinazoendana zaidi, muundo bora wa vali, na utunzaji bora wa mtiririko wa damu.
Mafanikio yamepatikana: utafiti mmoja uligundua asilimia 80% ya wagonjwa waliowekewa moyo wa bandia waliweza kuishi kwa zaidi ya mwaka mmoja, na wengine kwa miaka sita. Muda mrefu zaidi mgonjwa alisaidiwa kupandikizwa moyo ilikuwa siku 1,373. Lakini matatizo makubwa ya kuambukiza bado yalikuwa ya kawaida, na lengo la tiba kamili ya "marudio" kwa moyo wa bandia bado ilikuwa ndoto ya mbali.
Wakati huo huo, hitaji la dharura la upandikizaji wa juu lilikuwa limechukua teknolojia katika mwelekeo mwingine. Badala ya kuchukua nafasi ya moyo uliodhoofika kabisa, wazo lilikuwa kuweka sambamba na kuutegemeza kwa kusaidia mtiririko wa damu.
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Maelezo ya picha,
Robert Jarvik alitengeneza kifaa ambacho kingemfanya mgonjwa wa moyo kuishi kwa muda akisubiri kubadilishwa damu, lakini hakikuwa na mafanikio makubwa
Utafutaji wa moyo wa bandia usipandikizwa ndani ya mwili unaendelea. Kujaribu kuunda vitengo vya nje vya transcutaneous ili kutekeleza kikamilifu mahitaji ya moyo ndio changamoto kubwa zaidi kwa wanasayansi. Vipimo vya jumla vya moyo wa bandia huhitaji kusukuma lita nane (pinti 14) ya damu kwa dakika dhidi ya shinikizo la damu la 110mmHg (milimita za zebaki).
Suluhu inaonekana kuwa karibu sana, lakini hakuna anayetarajia safari hii kuwa rahisi. Kushindwa kufikia lengo kwa miaka mingi kumesababisha wanasayansi kuwa na unyenyekevu mkubwa na uhandisi wa asili wa moyo