Kigoma: Shule ya Mvinza Kagerankanda haina Madarasa na Madawati
Hii ni kwa shule hapo kigoma kwan kuna uhaba wa madarasa kama inavyoonekanaShule ya Msingi Muvinza iliyopo Kata ya Kagerankanda, Wilaya Kasulu Mkoani Kigoma ina changamoto ya upungufu mkubwa wa madarasa na madawati hali nayowafanya wanafunzi wengi kusoma nje na wengine kusoma wakiwa wamekaa chini katika madarasa machache yaliyopo.
Wanafunzi ambao wameanza elimu ya Msingi Mwaka 2023 shuleni hapo wanakaa chini kwa kuwa madarasa yamejaa, ikitokea kuna mvua inamaanisha siku hiyo hakutakuwa na masomo kwa wale wanaosomea nje.
Akizungumzia hali hiyo, Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Kasulu, Mbelwa Abdallah Chidebwe amesema shule ina Wanafunzi zaidi ya 2000 na ina madarasa mawili.
Amesema “Kuna madarasa mengine mawili ambayo Walimu walilazimika kuyageuza kuwa ofisi, lakini tayari ujenzi wa madarasa mengine unaendelea, jumla naweza kusema kuna upungufu wa madarasa zaidi ya 10.
“Kuhusu madarasa ambayo hayana madawati pia kuna mchakato unaendelea wa kuongeza madawati.”
MWALIMU MKUU
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kagerankenda, Zakalia Leganya Charles amekiri uwepo wa changamoto hizo za madawati na wanafunzi kukaa chini kisha akatoa takwimu:
Idadi ya Wanafunzi Awali Wavulana 44 Wasichana 60, darasa la Kwanza Wavulana 221 Wasichana 198 jumla 419.
Darasa la Pili Wavulana 122 Wasichana 137 Jumla 259, Darasa la Tatu Wavulana 298 Wasichana 251 Jumla 549.
Darasa la Nne Wavulana 189 Wasichana 202 Jumla 391, Darasa la Tano Wavulana 73 Wasichana 82 Jumla 155.
Darasa la Sita Wavulana 84 Wasichana 69 Jumla 153, Darasa la Saba Wavulana 28 Wasichana 26 Jumla 54.
Hivyo, Jumla kuna Wavulana 1059 Wasichana 1025 na kufanya jumla yao wote iwe 2084, Walimu waliopo 15, mahitaji ni Walimu 46, upane wa MEMKWA waliopo ni Wavulana 13 Wasichana 14, jumla yao ni 27.
Mahitaji ya madarasa na madawati
Madarasa mahitaji ni 46 yaliyopo 12, pungufu ni madarasa 34, yakikamilika manne yanayojengwa pungufu itakuwa madarasa 30.
Madawati mahitaji ni 694 yaliyopo ni 184 pungufu 510, vyoo mahitaji Wavulana 42 vilivyopo ni 10, Wasichana mahitaji matundu 51 yaliyopo ni 6 pungufu 45, mapungu kwa jumla ni matundu ya Wavulana 32 Wasichana 45, jumla 77, Nyumba za walimu mahitaji ni 46 zilizopo ni 7 pungufu 39
Je kama mdau wa elimu nini mapendekezo yako????