#HABARI Jeshi la polisi mkoani Kagera limefanikiwa kumkamata kijana Paschal Kaigwa (22) mzaliwa wa Kishogo Bukoba Vijijini, ambaye anatuhumiwa kumbaka na kumuua mke wa mwenyekiti wa mtaa wa National Housing kata ya Rwamishenye katika manispaa ya Bukoba, aitwaye Khadija Ismail (29)
Kamanda wa polisi mkoani Kagera William Mwampaghale amesema kuwa mtuhumiwa huyo alijificha katika vichaka na kwamba baada ya kukaa huko bila chakula, aliamua kutoka mafichoni na kwenda nyumbani kwa shangazi yake katika mtaa wa Katatorwansi ulioko katika manispaa ya Bukoba
Imeelezwa kuwa alipofika alikuta watoto ambao baada ya kumuona walipiga kelele na kuwezesha wananchi kumkamata.
"Njaa ilimtoa mafichoni akaenda kwa shangazi yake, lakini watoto aliowakuta pale walikuwa tayari wana taarifa, kutokana na taarifa zenu mlizozitangaza kuwa anatafutwa, tumemkamata juzi tarehe 19/02/2023 saa kumi jioni, tunaye tunamhoji na tutamfikisha kwenye vyombo vya kishera" amesema Kamanda Mwampaghale
#EastAfricaTV
Tags
LIFESTYLE