Hukumu kuhusu mwimbaji robert sylvester kelly(R.kelly)

 





Hukumu ya Mwimbaji Robert Sylvester Kelly (R.Kelly) ya kupatikana na hatia ya makosa ya kufanya unyanyasaji wa kijinsia, kutayarisha ponografia za Watoto pamoja na kushawishi Watoto hao kufanya vitendo vya ngono, inatarajiwa kusomwa leo Jijini Chicago nchini Marekani.


Inaripotiwa kuwa kwa hatia hiyo R.Kelly anaweza kuhukumiwa kifungo kisichopungua miaka 10 gerezani japo Waendesha mashtaka kwenye kesi hiyo wamemuomba Jaji wa Chicago atoe hukumu ya kifungo cha miaka 25 jela kwa Mwimbaji huyo ili iwe fundisho kwa wengine.


Tayari R.Kelly mwenye umri wa miaka 56 ameanza kutumikia kifungo cha miaka 30 jela ambacho alihukumiwa na Mahakama ya New York kwenye kesi ambayo ilijumuisha ushuhuda kutoka kwa Mashahidi ambao walisema walinyanyaswa kijinsia na Msanii huyo.


Kwenye kesi hiyo ya New York, pia Mahakama ilisikiliza ushuhuda kutoka kwa Watu waliohusika na kupanga ndoa ya Kelly na marehemu Aaliyah mwaka 1994 ikidaiwa aliolewa akiwa na miaka 15. #MillardAyoMAHAKAMANI

Picha zake 

Akiwa na vazi la gereza


Akiwa urahiani

Msomi wetu

Tembelea bloggers yetu kwa ajili ya kupata habari mbalimbali za michezo burudani elimu nakadhalika

1 Comments

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post